Dodoma FM

Apandishwa kizimbani kwa tuhuma za kuua

5 December 2020, 10:56 am

Na Zakia Ndulute,

Dodoma.

Mkazi wa Railway katika Wilaya ya Dodoma HAMALA DALA(32) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Dodoma kwa shitaka la kuua kwa kukusudia.
Akisomewa shitaka lake mbele ya Hakimu wa Wilaya ya Dodoma PASCHAL MAYUMBA na mwendesha mashitaka ambaye ni wakili wa Serikali SARARA MORICE amedai kuwa mnamo Novemba 17 mwaka huu katika eneo la Railway Dodoma Mshitakiwa alifanya tukio la mauaji ya kudhamiria.
Wakili wa Serikali ameongeza kuwa Mshitakiwa alifanya kitendo cha mauaji ya kukusudia kwa kumuua NEEMA AMOSI Kitendo ambacho ni kosa kisheria katika makosa ya jinai.
Hata hivyo wakili SARARA amesema kuwa upelelezi wa shitaka hilo bado haujakamilka na kumuomba Hakimu ataje tarehe ya kusikilizwa tena kesi hiyo.
Kwa upande wake Hakimu MAYUMBA ameieleza mahakama kuwa mshitakiwa haruhusiwi kusema chochote kwakuwa Mahakama ya Wilaya haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.
Mshitakiwa amerudishwa Rumande mpaka shauri lake litakapo tajwa tena Mahakamani hapo Disemba 18 mwaka huu.