Dodoma FM

Serikali yazindua kampeni ya kulinda maadili

16 May 2023, 10:56 am

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akizindua kampeni hiyo katika kongamano  maalum. Picha na Mariam Matundu.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amepongeza juhudi za Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalum kwa juhudi za kutoa za Elimuu juu ya umuhimu wa Familia na Upendo katika Jamii zetu.

Na Mariam Matundu.

Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Familia, Mei 15, 2023, Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imezindua Kampeni ya Kitaifa kuhakikisha maadili yanalindwa na kuendana na mila na desturi za nchi.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akizindua kampeni hiyo katika kongamano  maalum, amesema jamii yenyewe inatakiwa kuwajibika kwenye malezi yanayoendana na miiko na tamaduni za kitanzania ili kuimarisha familia na kuepuka mmomonyoko wa maadili.

Mhe. Dkt. Gwajima amebainisha kwamba takwimu za vitendo vya ukatili hasa kwa watoto zinaonesha asilimia 60 ukatili unafanyika nyumbani hivyo msingi wa kwanza katika kutelekeza kampeni hiyo ni kuanzia ndani ya familia.

Sauti ya Mhe. Dkt. Gwajima.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akiwa ameambatana na Viongozi mbalimbali wakikagua bidhaa mbalimbali. Picha na Mariam Matundu.

Awali mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ustawi na maendeleo ya jamii Fatma Toufiq amesema ili kuwa na bora na yenye ustawi ni muhimu familia ziwe na upendo na maadili pamoja na kumshirikisha Mungu.

Sauti ya Mwenyekiti wa kamati.

Nae mwakilishi wa IGP Mrakibu Msaidizi wa Polisi Dkt Ezekiel Kyogo amesema ni muhimu familia ziwekeze katika malezi ili kulinda maadili hali itakayo saidia vyombo vya ulinzi na usalama kupunguza mzigo wa kupambana na wahalifu  kwa kuwa taifa litakuwa na watu wenye maadili na uadilifu.

Sauti ya mwakilishi IGP .
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi. Rosemary Senyamule na Fatma Tawfiq wakikagua mabanda mbalimbali ya bidhaa wakati wa uzindduzi huo. Picha na Mariam Matundu.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amepongeza juhudi za Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalum kwa juhudi za kutoa za Elimuu juu ya umuhimu wa Familia na Upendo katika Jamii zetu.

kauli mbiu katika maadhimisho hayo ni” LINDA MAADILI NA UPENDO KWA FAMILIA IMARA”.