Dodoma FM

Walimu watakiwa kuboresha mazingira ya shule kwa kupanda miti

24 July 2023, 2:32 pm

Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ikikagua ujenzi wa zahanati kijiji cha Chilungulu.Picha na Bernad Magawa.

Na Bernad Magawa

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Bahi Mheshimiwa Donald Mejitii amewaagiza walimu wa shule za msingi wilayani Bahi kuhakikisha wanaboresha mazingira ya shule mpya zilizojengwa kupitia fedha za BOOST pamoja na zile za zamani kwa kupanda miti ya kutosha.

 Pia amewashauri kutenga maeneo ya kutosha kwa ajili ya kilimo ili watoto waweze kujifunza kazi za mikono ambazo zitawasaidia watakapohitimu masomo yao.

Mheshimiwa Mejitii ameyasema hayo wakati wa ziara ya kamati ya Fedha Uchumi na Mipango iliyotembelea miradi ya maendeleo katika siku ya kwanza ya ziara hiyo ambapo zaidi ya miradi mitano ilitembelewa huku akiwashukuru wananchi kwa kujitoa katika nguvu kazi na kupelekea miradi hiyo kukamilika kwa wakati na kuwa wa kwanza katika mkoa wa Dodoma.

Sauti ya Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Bahi.
Kamati ya fedha uongozi na mipango ikikagua matundu matatu ya vyoo katika shule ya msingi Msisi.Picha na Bernad Magawa.

Akizungumza kwa niaba wananchi Diwani wa kata ya Bahi Mheshimiwa Agostino Ndonuu, ameishukuru serikali kwa kupeleka miradi mingi wilayani humo huku walimu  wakiahidi kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na mwenyekiti wa halmashauri.

Sauti za Diwani na Mwalimu.