Dodoma FM

Nani anapaswa kumlipa dalali kati ya mpangaji na mwenye nyumba?

17 August 2023, 3:40 pm

Wakazi wa Jiji la Dodoma wamekuwa na maoni tofauti kuhusu nani anae paswa kumlipa dalali. Picha na Aisha Alim.

Biashara ya udalali inekuwa ikifanywa na baadhi ya watu kwa lengo la kujipatia kipato na kuendesha maisha yao.

Na Aisha Alim.

Utaratibu wa upatikanaji wa nyumba za biashara na nyumba za kuishi kupitia madalali umekuwa ukihusisha gharama za ulipwaji wa dalali anaewezesha kupatikana kwa vyumba hizo.

Jambo ambalo limeendelea kuleta mkanganyiko baina ya pande mbili kati ya mhitaji wa chumba hicho pamoja na mmiliki wa jengo ni nani anaepaswa kuwajibika kulipa gharama za dalali?

Juu ya swala hilo wananchi Jijini Dodoma wamekuwa na maoni tofauti wakieleza ni nani anaestahili kulipia gharama za udalali kati ya mpangaji na mmiliki wa nyumba

Sauti za wapangaji.
Dodoma Tv imepita katika baadhi ya mitaa ya jiji la Dodoma na kuwauliza wananchi, wenye nyumba na madalali swali hilo.Picha na Aisha Alim.

Dodoma Tv imemtafta dalali anayehusika na utaftaji wa vyumba vya kupangisha kwa ajili ya makazi na biashara ambapo amesema anayestahili kulipa gharama hizo ni mpangaji kutokana na uhitaji wake wa nyumba kwa muda huo

Sauti za Madalali.