Dodoma FM

Wakazi wa Handali walalamika kukosa maji safi na salama

16 October 2023, 6:44 pm

Picha ni Uchimbaji wa mradi huo wa maji katika eneo hilo. Picha na Mindi Joseph.

Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA wapo kwenye mpango wa bajeti katika  kuhakikisha miundombinu ya maji katika kijiji cha Handali inafufuliwa.

Na Mindi Joseph.

Kusimama kwa Mradi wa Maji unaogharimu zaidi ya Milioni 600 katika kijiji cha Handali Wilayani Chamwino imechangia wakazi wa eneo hilo kutumia maji yasiyo safi na salama.

Dodoma Tv imefanikiwa kufika katika Mradi huo na kushuhudia baadhi ya adha wanazopitia wananchi wa kijiji hicho ambapo inawalazimu kutembea umbali mrefu kutafuta maji safi na salama.

Picha ni Diwani wa Kata ya Idifu  Samwel Kawea.picha na Mindi Joseph.

Tumezungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii ambaye ni Diwani wa Kata ya Idifu  Samwel Kawea Kujua ni hatau zipi halmashauri wanachukua kuhakikisha wananchi wa kijiji hicho wanafanikiwa kupata huduma ya maji safi na salama.

Sauti ya bw.Samwel Kawea.

Katika kutatua changamoto hiyo ya Maji, Jumuiya ya watumiaji maji imeanzishwa katika Kijiji cha Handali .

Sauti ya bw.Samwel Kawea.