Dodoma FM

Wananchi mwatano walalamikia kero ya taka

10 August 2026, 16:43

Uhifadhi usio sahihi wa taka husababisha uchafuzi wa mazingira. Picha na mtandao

Wananchi hao wametakiwa kutambua kuwa elimu ni nyenzo muhimu katika kukabiliana na changamoto ya utunzaji wa mazingira, huku wakisisitizwa kujenga utamaduni wa kutupa taka katika maeneo maalumu na kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama.

Na Ramla Kimu.

Wananchi wa Mtaa wa Mwatano kata ya Miyuji wamelalamikia kero ya usambaaji wa taka katika maeneo yao hali hiyo inatokana na uhifadhi usio sahihi wa taka katika kiwanda cha ukusanyaji na urejeshaji wa taka kiwandani hapo.

Wakiongelea changamoto hiyo baadhi ya wananchi  wa mtaa huo wameiomba Serikali kuendelea kuimarisha vituo vya urejeshaji taka viwandani, pamoja na kuwezesha vituo hivyo kwa vifaa kama magari na mashine zinazoweza kurahisisha ukusanyaji na kupunguza wingi wa taka mitaani.

Akijibu tuhuma hizo za wananchi Meneja wa Kiwanda hicho, Bi.Zulfa Nassoro, amesema pamoja na changamoto zinazojitokeza, uanzishwaji wa kiwanda hicho una faida mbalimbali ikiwemo kuondoa taka katika mazingira, uzalishaji wa malighafi mpya pamoja na kutoa fursa za ajira kwa vijana.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mtaa huo, Bw. Jumanne Muumennya, amesisitiza umuhimu wa wananchi kushirikiana katika kuhakikisha taka zinahifadhiwa kwa utaratibu unaolinda mazingira na afya za wakazi wa eneo hilo.

Sauti na Ramla Kimu.