Wananchi Huzi walia na uvamizi wa tembo
17 August 2026, 17:35

Wananchi walio athiriwa na tembo hao kupewa fomu za kujaza na uongozi wa kijiji ili kufidiwa hasara waliyo ipata lakini hakuna utekelezaji wowote.
Na Victor Chigwada.
Wananchi wa kijiji cha Huzi Wilaya ya Chamwino wameiomba Serikali kuwasaidia kukabiliana na Tembo ambao wamekuwa wakivamia mashamba ya wakulima na kushambulia mazao yao.
Taswira ya habari imezungumza na baadhi ya wananchi hao ambapo wame kiri kukutana na mashambulizi ya tembo katika mashamba yao hali inayo chochea uhaba wa chakula.
Aidha wameongeza kuwa suala hilo wameendelea kulitolea taarifa lakini hadi sasa halijatatuliwa hivyo wanaiomba serikali kuingilia kati.
Yusuph Munjile Mwenyekiti wa kijiji cha Huzi amesema athari za wanyama hao zimepelekea wakati wingine wananchi wa kijiji hicho kuvuna mazao yao yakiwa bado hayajakomaa vizuri.