Dodoma FM
Dodoma FM
12 May 2026, 17:44

Kupanda kwa bei ya mafuta kumewaathiri kwa kiasi kikubwa kwani baadhi yao wamejikuta wakipokonywa pikipiki.
Na Firdaus.
Wananchi jijini Dodoma wamelalamikia kupanda kwa gharama za maisha hali inayopelekea biashara kukwama na maisha kuwa magumu.
Taswira ya habari imetembelea mitaa ya Chamwino na Chinangali jijini Dodoma na kuzungumza na wananchi mbalimbali wakiwemo wajasiriamali na bodaboda ambapo wamesema kwasasa hali imekuwa ngumu sana na baadhi ya watu wameanza kukata tamaa ya kuendelea na biashara.
Nao baadhi ya maafisa usafirishaji almaarufu kama bodaboda wakiongea na taswira ya habari wamesema kupanda kwa bei ya mafuta kumewaathiri kwa kiasi kikubwa kwani baadhi yao wamejikuta wakipokonywa pikipiki za mikataba na wamiliki baada ya kushindwa kurejesha hesabu kamili.