Dodoma FM

Mlimwa walalamikia upungufu wa huduma ya maji

2 August 2023, 2:59 pm

Wananchi hao wanasema wanalazimika kutumia maji ambayo si safi na salama. Picha na Mulika.

Ngulelo amesema kuwa hali hiyo inawalazimu kutumia maji ambayo si safi na salama na kuiomba Serikali kuingili kati suala hilo.

Na Victor Chigwada.

Wananchi wa kijiji cha Mlimwa  wilayani Chamwino wamelalamikia changamoto ya upungufu wa huduma ya maji hali inayowapa wakati mgumu Wazee,watu wenye Ulemavu na wanawake.

Wakizungumza  na Taswira ya Habari baadhi ya wananchi wameiomba Wakala wa Usambazaji  maji vijijini RUWASA kuwasaidia kuwapeleka mradi wa maji utakaosaidia kutatua adha hiyo.

Sauti za wananchi wa Mlimwa.

Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw.Musa Ngulelo amesema kuwa kisima kilichopo hakikidhi mahitaji ya vitongoji vyote hali inayosababisha baadhi ya wananchi kutembea umbali mrefu.

Sauti ya Mwenyekiti.

Ngulelo ameongeza kuwa hali hiyo inawalazimu kutumia maji ambayo si safi na salama na kuiomba Serikali kuingili kati suala hilo

Sauti ya Mwenyekiti.
Wananchi wameiomba Wakala wa Usambazaji  maji vijijini RUWASA kuwasaidia kuwapeleka mradi wa maji utakaosaidia kutatua adha hiyo. Picha na Mulika.

Simoni Macheho ni  Diwani wa Kata ya Membe amesema tayari kijiji cha Mlimwa kipo kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 ili kuondokana  na changamoto ya maji

Sauti ya Diwani.