Dodoma FM

UCSAF kupeleka mawasiliano katika kata 1900 Nchini

27 September 2023, 3:21 pm

Picha ni mnara wa mawasiliano ya simu . Picha na UCSAF.

Mfuko wa Mawasiliano kwa wote UCSAF umeendelea na jitihada za kuhakikisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano ambapo kwa kpindi cha mwaka mmoja julai 2022 hadi june 2023 umejenga minara 304.

Na Mariam Matundu.

Mfuko wa mawasiliano kwa wote UCSAF umesaini mikataba ya kupeleka mawasiliano katika kata zaidi ya 1900 Nchini ambapo itawezesha watanzania milioni 15 kupata huduma ya mawasiliano.

Mtendaji Mkuu wa UCSAF Justina Mashiba ameeleza kwamba utelekezaji wa mradi huo mpaka sasa umefikia asilimia tisini ambao umewezeshwa na serikali kwa kushirikiana na watoa huduma za mawasiliano.

Sauti ya Bi Justina Mashiba.
Mfuko huo pia umewezesha shule ya msingi Samia Suluhu kupata Vifaa vya TEHAMA.Picha na UCSAF.

Adha amesema katika kuboresha mazingira ya wananchi wanaohamia katika kijiji cha Mkababu Msomera kutoka Ngorongoro tayari UCSAF kwa kushirikiana na TTCL wamepaleka huduma ya mawasiliana katika kijiji hicho.

Sauti ya Bi. Justina Mashiba.

katika hatua nyengine mfuko huo umewezesha shule ya msingi Samia Suluhu kupata Vifaa vya TEHAMA ikwemo Komptyuta na Projekta.

Sauti ya Bi. Justina Mashiba.