Dodoma FM

Shule ya sekondari Amani Abeid yamkosha Senyamule

13 July 2023, 4:10 pm

Wanafunzi wa shule ya sekondari Amani Abeid Karume iliyopo katika kata ya Pahi ilaya ya Kondoa.Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Wanafunzi wametakiwa kusoma kwa bidii ili kukutana na fursa nyingine za kielimu.

Na Fred Cheti

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amekoshwa na ufaulu wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Amani Abeid Karume iliyopo katika kata ya Pahi wilaya ya Kondoa.

Mhe. Senyamule ameyasema hayo wakati akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo akiwa wilayani humo katika ziara yake ya kikazi ambapo ameipongeza shule hiyo iliyofanya vizuri kwa asilimia mia moja katika mtihani wa kidato cha sita uliopita.

Sauti ya mkuu wa Mkoa.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma mh. Rosemary Senyamule akizungumza wilayani Kondoa. Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Aidha Mhe. Senyamule amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii ili kukutana na fursa zingine za kielimu kwani serikali inaendelea kuboresha mazingira ya elimu ikiwemo ujenzi wa vyuo vya ufundi mkoani Dodoma pamoja  wa miundombinu mingine

Sauti ya Mkuu wa Mkoa.