Dodoma FM

BMH yafanikiwa kupandikiza Uroto kwa watoto 7

31 January 2024, 7:05 am

Picha ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospital ya Benjamin Mkapa Alphonce Chandika akiongea na waanishi wa habari. Picha na Yussuph Hassan.

Itakumbukwa kuwa Serikali ya awamu ya sita iliidhinisha Shiling Bilioni 3.6 kwa kuwezesha kutolewa kwa huduma za upandikizaji wa uroto kwa Watoto wenye selimundu huku zikitengwa Shiling Bilioni 1 kwa ajili ya kutoa kwa Watoto bure.

Na Yussuph Hassan.
Hospital ya Benjamin Mkapa Dodoma, imefanikiwa kupandikiza Uroto kwa Watoto 7 walikuwa wakisumbuliwa na ugonjwa wa Selimundu huku tiba hiyo ikitajwa kuwa bora zaidi kwa ugonjwa wa selimundu.

Imeelezwa kuwa asilimia 50 ya Watoto wanaozaliwa na Ugonjwa wa Selimundu hawafikishi miaka 5 huku wanaosalia huendelea na matibabu yanayowagharimu kwa maisha yote.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma Mkurugenzi Mtendaji wa Hospital ya Benjamin Mkapa Dkt.Alphonce Chandika amesema kuwa tiba ya kawaida imekuwa na gharama kubwa ukilinganisha na upandikizaji uroto.

Sauti ya Dkt.Alphonce Chandika.
Picha ni Hospitali ya Benjamin Mkapa . Picha na Yussuph Hassan.

Aidha Dkt Chandika ameainisha Takwimu za ugonjwa huo kwa Afrika Tanzania ikiwa ni Nchi ya tatu, na ulimwenguni ni Nchi ya nne kwa kuwa na Watoto wengi wenye Selimundu.

Sauti ya Dkt.Alphonce Chandika.

Mzee Joseph John ni moja kati Wazazi wa Watoto waliopatiwa Tiba ya uroto na hapa anazungumzia hali ilivyokuwa kwa Mtoto wake.

Sauti ya Mzazi.