Dodoma FM

Maeneo ya ukusanyaji taka jijini Dodoma yatakiwa kuboreshwa

15 September 2023, 8:25 am

Akikagua maeneo ya kukusanyia taka ndani ya jiji la Dodoma.Picha na David Kavindi.

Ukaguzi wa maeneo ya kuhifadhia taka ndani ya jiji la dodoma umefanywa na mkuu wa wilaya hiyo bw. Jabir shekimweri ikiwemo maeneo ya nguhungu, changombe, miyuji pamoja na eneo la chidaji sehemu ya mwisho ya kuzika taka ngumu. 

Na David Kavindi.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mh. Jabir shekimweri amemuagiza mkuu wa kitengo cha usimamizi wa taka ngumu na usafi wa mazingira katika halmashauri ya jiji la dodoma kuboresha maeneo ya ukusanyaji wa taka ndani ya jiji.

Ametoa maelekezo hayo wakati akikagua maeneo ya kukusanyia taka ndani ya jiji la Dodoma ambapo amesema serikali ina wajibu wa kushirikiana na Taasisi ya Sido pamoja na wadau wa mazingira kuwezesha uchakataji wa taka kabla ya kufikishwa katika dampo kuu la chidachi.

Sauti ya Mh. Jabir Shekimweri.
Picha ni gari la kubeba taka .Picha na Thadei Tesha.

Nae Peter Madono meneja wa dampo la chidaya jijini Dodoma amesema changamoto ya barabara na uchakavu wa mitambo imekuwa ikisababisha kushindwa kufanya kazi ya uchakataji wa taka hizo kwa ufanisi.

Sauti ya Peter Meneja wa Dampo.