Dodoma FM

Tembo wakatisha  vikao vya maendele ya kijiji Chinugulu

14 Aprili 2026, 18:34

Uwepo wa tembo katika maeneo hayo umesababisha maafa ya mara kwa mara.Picha na mtandao.

Inaelezwa kuwa vitongoji hivyo vilivyo karibu na pori hilo la akiba havifikiwi na viongozi wake mara kwa mara.

Na Victor Chigwada.

Viongozi wa Kijiji cha Chinugulu wilayani Chamwino wameeleza kushindwa kuvifikia baadhi ya vitongoji wanavyo viongoza kutokana na uwepo wa tembo katika pori la akiba la Lunda Mkwambi wanao tishia usalama wao.

Inaelezwa kuwa vitongoji hivyo vilivyo karibu na pori hilo la akiba havifikiwi na viongozi wake mara kwa mara pia hakuna mikutano ya maendeleo inayo fanyika kwa kuogopa kuvamiwa na Tembo hao.

Akiongea na taswira ya habari mwenyekiti wa kijiji cha Chinugulu Bw. .Daniel Njelula amesema kwasasa wanyama hao wamepungua kutokana na mvua nyingi zilizo nyesha hivi karibuni lakini pindi maji yanapo pungua katika mto kizigo uliopo mpaka mwa hifadhi ya Ruaha hurudi Tena kuvamia mashamba na makazi ya wananchi .

Sauti ya Bw. .Daniel Njelula

Njelula amekiri kuwa uwepo wa tembo katika maeneo hayo umesababisha maafa ya mara kwa mara ambapo mwaka 2025 tembo walivamia vitongoji hivyo na kuharibu mashamba, makazi ya watu pamoja na kusababisha vifo vya baadhi ya wananchi.

Sauti ya Bw. .Daniel Njelula

Nao baadhi ya wakazi wa kitongoji cha Chinyika wameiomba Serikali kujenga vituo vya askari wa wanyama pori Ili kusaidia kukabiliana na adha hiyo.

Sauti za wananchi.