Dodoma FM

Wanawake watakiwa kujikita katika shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato

14 July 2026, 17:18

Picha ni mmoja kati ya wanawake anae jishughulisha na ufundi wa ujenzi.Picha na Anwary Shaban.

Kadiri wanawake wanavyoendelea kuvunja vikwazo na kushiriki katika sekta mbalimbali za uzalishaji, wito unatolewa kwa jamii kuendelea kuwaunga mkono na kuwapa fursa sawa, ili uwezo wao uweze kuchangia maendeleo ya familia, jamii na taifa kwa ujumla.

Na Anwary Shaban.

Wanawake wametakiwa kujikita katika shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato na kuacha dhana ya kuamini baadhi ya kazi ni za wanaume pekee.

Kwa muda mrefu kazi za ujenzi (Ufundi uashi )imekuwa ikiaminiwa kuwa ni kazi ya  wanaume pekee, wanawake walio thubutu kufanya kazi hii walijikuta wakichukuliwa tofauti na jamii lakini sasa hali imebadilika baadhi ya wanawake wameanza kujihusisha na kazi hii .

Nimetembelea katika moja ya eneo linalo fanyika kazi ya ujenzi wa nyumba katika mtaa wa Miyuji Proper jijini Dodoma na hapa nakutana na mafundi mbalimbali wakiwemo wanawake wakiwa wanaendelea na kazi ya ujenzi .

Nawauliza nini kiliwasukuma kujiingiza katika kazi hii ya ujenzi licha ya mitazamo mbalimbali ambayo wamekuwa wakikutana nayo katika jamii juu ya wanawake kujihusisha na kazi zinazo aminiwa kuwa ni za wanaume pekee.

Aidha, wanawake hao wamewataka wanawake wengine wanaokaa nyumbani wakisubiri kuajiriwa au wanaochagua kazi kuachana na mtazamo huo, badala yake wajitokeze kufanya kazi yoyote halali inayoweza kuwaingizia kipato na kuwainua kiuchumi.

Msafiri Charles ni fundi mwenye uzoefu wa takribani miaka 27 yeye anasema wanawake wanapopewa nafasi katika sekta ya ujenzi huonyesha bidii na uwajibikaji mkubwa.

Picha ni mmoja kati ya wanawake anae jishughulisha na ufundi wa ujenzi.Picha na Anwary Shaban.

Naye mhandisi wa majengo, Ramadhan Salumu, amesema wanawake wameendelea kutoa mchango mkubwa katika sekta ya ujenzi kutokana na nidhamu, umakini na kujituma kwao. Hata hivyo, ameeleza kuwa bado wanakabiliwa na changamoto zinazotokana na mitazamo hasi ya baadhi ya watu, na kuitaka jamii kuachana na dhana kuwa ujenzi ni kazi inayowahusu wanaume pekee.

Sauti ya Anwary Kina.