Adha ya maji Mwenzele wananchi wachangia vyanzo vya maji na wanyama
6 July 2026, 16:40

Wananchi wa Mwezele wameiomba Serikali kuharakisha utekelezaji wa miradi hiyo ili waweze kupata huduma ya maji safi na salama.
Na Stephen Noel.
Wananchi wa Kijiji cha Mwezele, Kata ya Mwezele Wilaya ya Mpwapwa, Mkoani Dodoma, wanasema maisha yao yamekuwa magumu kutokana na adha ya upatikanaji wa maji safi na salama.
Hali hiyo imepelekea wananchi hao kuchangia vyanzo vya maji na wanyama, jambo linalochangia kuongezeka kwa magonjwa.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwezele, Bw. Festo Mgohachi, amesema changamoto hiyo imedumu kwa miaka mingi na imeathiri afya na maendeleo ya wakazi wa kijiji hicho.
Kwa upande wake, Afisa Afya Wilaya ya Mpwapwa, Bi. Mary Mabangwa, amethibitisha kuwepo kwa changamoto hiyo.
Amesema wananchi wengi wa Mwezele wamekuwa wakipata magonjwa yanayotokana na maji machafu kama kichocho, kipindupindu na magonjwa ya kuharisha.