Dodoma FM

Wananchi jijini Dodoma wametakiwa kutunza miundombinu ya maji taka

24 September 2021, 9:08 am

Na; Thadey Tesha.

Wito umetolewa kwa wananchi jijini Dodoma kutunza miundombinu ya maji hususani ya maji taka ili kuepuka athari za kiafya zinazoweza kujitokeza.

Wito huo umetolewa na MwenyeKiti wa mtaa wa Kiwanja ch ndege Bw. Ignas Joseph baada ya Serikali kuanza kuboresha miundombinu ya maji taka katika mtaa huo ambapo amesema kukamilika kwa maboresho hayo kutasaidia kupunguza athari za kiafya zilizokuwa zikisababishwa na maji kutuama katika mitaa hiyo.

Aidha wametoa wito kwa wananchi wa mtaa huo kuacha tabia ya kufungulia ovyo maji taka mtaani hapo kwani kwa kufanya hivyo hupelekea athari mbalimbali za kiafya ikiwemo magonjwa ya mlipuko.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wamesema kuwa suala la maji taka limekuwa kero mtaani hapo kwa muda mrefu ambapo wameishukuru Serikali kwa kulishughulikia suala hilo huku wakiahidi kuitunza miundombinu hiyo.

Serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya maji katika mitaa mbalimbali ambapo miongoni mwa mitaa iliyofaidika na maboresho hayo ni mtaa wa Kiwanja cha ndege, area c Jijini Dodoma ambapo maboresho ya mfumo mzuri wa maji taka yanaendelea.