Dodoma FM

Kushuka kwa bei ya mchele neema kwa walaji

30 April 2021, 12:59 pm

Na; Salim Kimbesi.

Imeelezwa kuwa kwa sasa bei ya mchele imeshuka sana sokoni kutokana na zao hilo kupatikana kwa wingi.

Hayo yamesemwa na wafanyabiashara wa mchele walipo kuwa wakizungumza na Dodoma fm ambapo wamesema mchele kwa sasa unapatikana kwa wingi hivyo kupelekea bei  kuwa chini tofauti na vipindi vingine.

Kwa upande wa walaji wao wanasema kushuka kwa bei ya mchele ni neema kwao kwani wanapata urahisi katika kununua na kutumia bidhaa chakula hicho.

Kushuka kwa bei ya mchele imekuwa faida kubwa kwa walaji hususani kipindi hiki cha mwezi mtukufu  wa ramadhani kwani imesaidia familia nyingi kujipatia mchele kwa urahisi zaidi.