Dodoma FM

Uhaba wa skimu za umwagiliaji watajwa kuchangia maisha duni

18 October 2022, 6:55 am

Na;Mindi Joseph .

Ukosefu wa Skimu za umwagiliaji katika baadhi ya maeneo Mkoani Dodoma umetajwa kuchangia Maisha Duni kwa wananchi kutokana na uzalishaji hafifu wa Chakula.

Taswira ya Habari imezungumza na Baadhi ya wanachi wa Kijiji cha Chunyu Wilayani mpwapwa ambapo wamebainisha kuwa kukosekana kwa skimu hizo imesababisha hali ya uzalishaji kuwa hafifu kutokana na baadhi yao kutegemea kwa kiasi kikubwa Mvua.

Wameongeza kuwa hali hiyo imechangia maisha yao kuwa Duni na kushindwa kujikwamu kiuchumi kupitia kilimo.

.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Chunyu Abineli Masila amesema wananchi wake wanahitaji kulima kilimo cha umwagiliaji na ameishukuru serikali kwa jitihada inazofanya ili kutatua changamoto hiyo inayowakabilii.

.