Dodoma FM

Migogoro baina ya viongozi Bolisa yazorotesha maendeleo

18 April 2023, 1:24 pm

Mbunge wa Jimbo la Kondoa mjini Mh. Makoa akizungumza na wakazi wa Bolisa. Picha na Nizar Mafita.

Katibu wa jumuiya ya wazazi wa chama cha mapinduzi wilayani humo amekemea mwenendo wa migogoro hiyo kwani itawagharimu katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa.

Na Nizar Mafita.

Migogoro na maslahi binafsi ya viongozi na wananchi katika Kata ya Bolisa Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma imetajwa kuchochea ucheleweshwaji wa miradi ya maendeleo katika Kata hiyo

Mbunge huyo akiwa katika ziara ya siku moja ndani ya kata ya bolisa wilayani kondoa amebaini migogoro baina ya viongozi wa chama na kata huku wananchi wakitajwa kuchangia uwepo wa migogoro hiyo ikiwemo mvutano uliopo baina ya wananchi juu ya mtaa gani unapaswa kujengwa majengo ya shule.

Sauti ya Mbunge wa jimbo la Kondoa mjini

Wakizungumza mbele ya mbunge huyo baadhi ya wananchi wa kata bolisa wamesema changamoto kubwa inaanzia kwa uongozi wa ngazi ya juu ndani ya kata.

Sauti za wakazi wa Bolisa
Wakazi wa Bolisa wakiwa katika mkutano huo. Picha na Nizar Mafita.

Kwa upande wake diwani wakata hiyo Ramla Abeid amesema hana mgogoro wowote kati yake na wananchi wala mbunge.

Sauti ya Diwani wa kata ya Bolisa