Dodoma FM

Taasisi Jijini Dodoma zahimizwa kufuatilia upandaji na ukuaji wa miti

12 April 2021, 12:05 pm

Na; Benard Filbert.

Taasisi zinazojihusisha na upandaji wa miti katika kukijanisha jiji la Dodoma zimetakiwa kuhakikisha zinapanda na kufuatilia ili kujua maendeleo ya miti hiyo.

Hayo yanajiri kufuatia taasisi mbalimbali kushiriki katika kampeni ya kukijanisha jiji la Dodoma kwa kupanda miti katika maeneo mbalimbali ya wazi.

Taswira ya habari imezungumza na afisa maliasili wa jiji la Dodoma Bw.Vedastus Miringa,ambaye amesema kila taasisi ambayo inapanda miti jijini hapa inatakiwa kuhakikisha inafuatilia ili kujua kama ya miti hiyo ni mazuri.

Amesema ofisi ya mazingira pamoja na maliasili katika jiji la Dodoma pia, wamekuwa wakifuatilia ili kujua maendeleo ya miti hiyo.

Hivi karibuni meneja mawasiliano wa Shirika la mazingira Duniani WWF Joanet Hanisa aliiambia taswira ya habari kuwa Shirika hilolilipanda miti zaidi ya300 katika Chuo Kikuu cha Dodoma lengo likiwa kuunga mkono juhudi za Serikali huku shirika hilo likiwekeza zaidi katika kutoa elimu kwa vijana kufanya ufuatiliaji  wa miti hiyo baada ya kuipanda.

Zoezi la upandaji wa miti katika jiji la Dodoma likihusisha taasisi mbalimbali lilianza mwaka 2017 lengo likiwa kukijanisha jiji la Dodoma.