Dodoma FM

Vyombo vya habari vyatakiwa kushiriki kutatua changamoto za uchaguzi

30 April 2024, 7:29 pm

Kongamano hilo limefanyika chini ya kaulimbiu isemayo Uandishi wa Habari za Uchaguzi kwa weledi hujenga USAWA, HAKI na UWAJIBIKAJI.

Na Pius Jayunga.
Waziri mkuu mstaafu na makamu wa rais Jaji Joseph Sinde Warioba amevitaka Vyombo vya Habari nchini kushiriki katika kusaidia katika kutatua changamoto zinazotokana na uchaguzi ili kujenga Demokrasia ya kweli.
Ametoa wito huo wakati akihutubia katika kongamano la wadau wa Habari lililofanyika Jijini Dodoma ambapo amesema si sahihi kwa Vyombo vya Habari kutegemea kuibua makosa yanayotokea wakati wa uchaguzi badala ya kushiriki kudhibiti makosa hayo yasiweze kutokea.

Sauti ya Jaji Joseph Sinde Warioba.

Msemaji mkuu wa serikali Mobale Mantinyi amesema msingi wa uadilifu wa Vyombo vya Habari katika kuripoti kwa usawa habari zote zinazohusu maswala ya uchaguzi itasaidia kuimarisha Demokrasia nchini.

Sauti ya Mobale Mantinyi .
Picha ni washiriki wa mkutano huo uliofanyika jijini Dodoma leo hii.Picha na Pius Jayunga.

Mwakilishi wa Rais baraza la Habari Tanzania Joyce Bazila amesema ni wajibu wa Vyombo vya Habari kudhibiti taarifa potofu kwa wananchi katika kipindi cha uchaguzi.

Sauti ya Joyce Bazila

Awali Katibu mtendaji wa baraza la Habari Tanzania MCT Ernest Sungura amesema kongamano hilo limelenga kuongeza Elimu kwa wapiga kura ili kufanya maamuzi sahihi wakati wa kupiga kura.

Sauti ya Ernest Sungura