Dodoma FM

Matumizi ya vyoo visivyo bora yatajwa kuchangia maambukizi ya kipindupindu

15 January 2024, 9:13 pm

Picha ni Afisa Afya Mkoa wa Dodoma Nelson Rumbeli akiongea na Dodoma Tv. Picha na Yussuph Hassan.

Pia inaelezwa kuwa ili mtu apate kipundupindu ni lazima awe amekula chakula au maji yaliyochafuliwa na vimelea vya ugonjwa huo .

Na Yussuph Hassan.
Ikiwa ni mwendelezo wa kutazama namna jamii inavyoweza kujikinga na magojwa ya mlipuko hasa kipindupindu, inaelezwa kuwa kutokutumia vyoo bora katika jamii ni moja ya tabia hatarishi za kupata ugonjwa huo.

Hayo yamesemwa na Afisa Afya Mkoa wa Dodoma Nelson Rumbeli wakati akifanya mahojiano maalum na Dodoma Tv kuhusu Ugonjwa wa Kipundipindu na Namna jamii inavyotakiwa kujikinga na maradhi hayo.