Dodoma FM

Ujenzi wa daraja la Ng’ong’ona kufungua fursa za kiuchumi

3 April 2024, 6:02 pm

Picha ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Ng’ong’ona Bwn Aizaki William Mpali wakati akizungumzia maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo.Picha na Fred Cheti.

Mikakati ya TARURA kuboresha Miundombinu ya barabara na madaraja katika mkoa wa Dodoma ili kurahisisha shughuli za kiuchumi.

Na Fred Cheti.
Ujenzi wa daraja la Ng’o’ng’ona lililopo katika Kata ya Ng’o’ng’ona Jijini Dodoma linalojengwa kwa teknolojia ya Mawe linatarajiwa kufungua fursa za kiuchumi kwa wananchi wa kata hiyo hasa waishio mtaa wa Ng’ong’ona.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Ng’ong’ona Bwn Aizaki William Mpali wakati akizungumzia maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo linalojengwa na Wakala wa barabara za vijijini na Mijini Tarura.

Sauti ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Ng’ong’ona.

Nao Baadhi ya wananchi katika Mtaa huo wameeleza furaha yao kutokana na ujenzi wa daraja hilo ambapo wamesema kukamilika kwake kutaleta tija kwa sababu kulikua na usumbufu wa mzunguko wa biashara kutokana na daraja hilo kuwa kiunganishi kikubwa cha mitaa mingine.

Sauti za Baadhi ya wananchi .

Kwa upande wake Meneja wa wakala wa barabara za Vijijini na Mijini (TARURA ) Mkoa wa Dodoma Bwana

Edward Lumelo amesema Mikakati ya TARURA kuboresha Miundombinu ya barabara na madaraja katika mkoa wa Dodoma ni kurahisisha shughuli za kiuchumi ambapo wanatumia teknolojia mbalimbali katika ujenzi huo ikiwemo mawe ili kupunguza gharama.

Sauti ya Bwana Edward Lumelo.