Dodoma FM

Utupaji wa taka ngumu katika mifumo ya maji taka wachangia kuziba kwa mifumo

26 March 2024, 7:13 pm

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph (kulia) akiwa na Diwani wa Kata ya Majengo, Shufaa Ibrahim wakikagua miundombinu ya majitaka katika eneo hilo.Picha na Seleman Kodima.

Mhandishi Aron Joseph akiwa sambamba na wataalamu kutoka Mamlaka hiyo na Viongozi wa kata hiyo kufanya Ziara katika mtaa huo ambao unakabiliwa na changamoto ya kuziba kwa mifumo ya maji taka .

Na Seleman Kodima.
Utupaji taka ovyo katika mifumo ya maji taka katika mtaa wa kitenge ,Bahi road kata ya Majengo umetajwa kuwa ni kikwazo mojawapo kinachosababisha uwepo wa changamoto za mara kwa mara katika mfumo wa maji taka eneo hilo.
Hayo yamebainika baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira DUWASA Mhandishi Aron Joseph akiwa sambamba na wataalamu kutoka Mamlaka hiyo na Viongozi wa kata hiyo kufanya Ziara katika mtaa huo ambao unakabiliwa na changamoto ya kuziba kwa mifumo ya maji taka .
Akizungumza baada ya kutembelea maeneo yenye changamoto hiyo,Mhandisi Aron amewasihi wananchi wa mtaa huo kuzingatia matumizi sahihi ya mifumo ya maji taka na kuacha kutupa taka ngumu katika mifumo hiyo.

Sauti ya Mhandishi Aron Joseph.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph (kushoto) akimpa maelezo Diwani wa Kata ya Majengo, Shufaa Ibrahim (wa pili kulia) namna taka ngumu zinazosababisha uzibaji wa chemba za majitaka.Picha na Seleman Kodima.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Mhandisi Benard Rugayi amesema licha ya DUWASA kuendelea kazi ya kuzibua chemba katika barabara inayojengwa katika mtaa huo bado wananchi wa mtaa huo wamekuwa ni sehemu ya changamoto .

Sauti ya Mhandisi Benard Rugayi .

Nae Diwani wa Kata ya Majengo Bi Shufaa Ibrahim amesema baada ya kubaini sababu za kuziba mara kwa mara kwa mifumo ya maji taka ndani ya mtaa huo watachukua hatua ya kuitisha mkutano wa mtaa ili kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya mifumo hiyo.

Sauti ya Diwani wa Kata ya Majengo Bi Shufaa Ibrahim .

Pamoja na hayo Viongozi wa mtaa huo akiwamo mtendaji wa mtaa kitenge Bi zuwena Jabu na Mwenyekiti wa Ccm tawi la Bahirodi Sungura Mohamed wameshukurua hatua zilizochukuliwa na DUWASA kuhusu changamoto hiyo na wameahidi kutoa elimu kwa wananchi wao.

Sauti za Viongozi wa mtaa huo .