Dodoma FM

Wanawake na fursa za kiuchumi

26 November 2020, 7:19 am

Wanawake nchini wameshauriwa kujishughulisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi ili kujiongezea kipato ambacho kitawasaidia katika mambo mbalimbali hususan katika kugombea na kuendesha kampeni wakati wa chaguzi. Ushauri huo umetolewa na mwenyekiti wa umoja wa wanawake Tanzania UWT mkoa wa Dodoma Neema Majole ikiwa ni wiki kadhaa tangu uchaguzi mkuu ufanyike oktoba 28 mwaka huu. Amesema kipato kwa mwanamke ndio silaha kubwa inayoweza kumuweka katika kuthubutu na kugombea kwenye nafasi za uongozi.