Dodoma FM

Jamii yatakiwa kuwapa wanawake kipaumbele cha kumiliki rasilimali

6 September 2021, 11:38 am

Na;Yussuph Hans.

Imeelezwa kuwa Wanawake wamekuwa na Mchango mkubwa katika familia, Jamii ikiwapa kipaumbele cha kumiliki Rasilimali.

Hayo yamebainishwa na Afisa Maendeleo ya Vijana Halmashauri ya Jiji la Dodoma Bw Mfungo Manyama wakati akizungumza na kituo hiki ambapo amesema ni muhimu jamii ikatoa fursa sawa ya umiliki wa rasimali ili kujenga Uchumi bora.

Taswira ya habari imezumguza na baadhi ya Wakazi Mkoani hapa kufahamu mtazamo wao juu ya Wanawake kumiliki rasilimali na kusema kuwa kundi hilo limekuwa likifanya jitihada kubwa kukuza uchumi wao licha ya baadhi ya changamoto wanazokabaliana nazo katika jamii.

Kwa upande wake Afisa Mipango kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania Flora Ndaba amesema kuwa changamoto inayomkandamiza Mwanamke kwenye kumiliki rasilimali ni kutopewa nafasi ya kutoa maamuzi suala ambalo linawakatisha tamaa.

Kuwapatia wananawake haki sawa za kumiliki mali kuna maanisha kupunguza vitisho vya unyanyapaaji, migogoro ya kifamilia na kijamii na ukiukwaji mwingine wa haki za binadamu, pia ni mchango chanya katika kuhusisha wanawake katika uchumi na kuwawezesha wanawake kwa ujumla.