Dodoma FM

Watoto wenye mahitaji maalum hawatakiwi kufichwa ndani

31 January 2024, 9:06 pm

Picha ni shule ya Msingi Viwizi iliyopo Dodoma Makulu Jijini Dodoma. Picha na Halmashauri ya jiji la Dodoma.

Shule ya msingi Dodoma Viziwi ni taasisi binafsi iliyoanzishwa mwaka 2005 ikiwa na jumla ya wanafunzi watano ambapo uandikishaji wa wanafunzi katika shule hiyo umezidi kuongezeka na katika mwaka huu 2024 imeandikisha jumla ya wanafunzi 22.

Na Fed Cheti.
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Alhaj Jabir Shekimweri amewataka wazazi na walezi kuacha tabia ya kuwaficha watoto wenye mahitaji maalum badala yake wawapeleke katika taasisi na vituo vinavyotoa mafunzo ili weweze kuwa na uwezo wa kujitegemea.

Mhe. Shekimweri ameyasema hayo mara baada ya kutembelea katika shule ya Msingi Viwizi iliyopo Dodoma Makulu inayofundisha watoto wenye matatizo ya kusikia ambapo amepongeza uongozi wa shule hiyo kwa hatua hiyo kubwa hasa katika kuwafundisha masomo watoto hao ikiwemo Masomo ya Amali.

Sauti ya Mhe. Shekimweri
Picha ni Mkuu wa wilaya pamoja na wadau wengine wakikagua vifaa mbalimbali katika shule hiyo.Picha na Halmashauri ya jiji la Dodoma.

Aidha Mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa serikali ya Mkoa wa Dodoma itaendelea kutoa ushirikiano kwa taasisi na vituo vinavyotoa mafunzo kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu ili kuhakikisha hakuna mtoto mwenye changamoto yoyote anaachwa kielimu.

Sauti ya Mhe. Shekimweri .

Kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo Mwl Awadhi Mbogo ameushuruku uongozi wa wilaya na Mkoa wa Dodoma kwa kunesha nia ya kushirikia na taasisi hiyo katika kuhakikisha kila mtoto wa kitanzania anapata haki yake ya Msingi.

Sauti ya Mwl Awadhi Mbogo .