Dodoma FM

Wafanyabiashara Majengo wapongeza kuimarika kwa usafi

19 September 2023, 5:18 pm

Picha ni baadhi ya wafanyabiashara wadogo wadogo wakiuza bidhaa nje ya soko hilo.Picha na Nipashe.

Usafi katika Soko hilo umesaidia kuendelea kuepukana na Magonjwa mbalimbali ya Mlipuko yatokanayo na uchafu.

Na Mindi Joseph.
Wafanyabiashara katika soko kuu la Majengo wamesema hali ya usafi imeimarika katika soko hilo kufuatia kuwepo kwa eneo maalum la kuweka takataka.

Baadhi ya wafanyabiashara wamesema asilimia kubwa wanazingitia sehemu za kuhifadhia takataka pasipo kutupa ovyo.

Wameongeza kuwa wale ambao wanatupa taka ovyo wamekuwa wakiwachukulia sheria ndogo pamoja na elimu.

Sauti za wafanyabiashara .