Dodoma FM

Utiaji saini makabidhiano mradi wa maji kutoka RUWASA kwenda DUWASA

9 June 2023, 3:22 pm

Mkurugenzi huduma kwa wateja mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Dodoma DUWASA Mhandisi Lena Mwakisale kushoto) na Kaimu meneja wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini RUWASA Mhandisi Mohamed Ally (kulia) wakikabidhiana taarifa za miradi ya maji. Picha na Bernadetha Mwakilabi.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Kongwa Mheshimiwa White Zuberi amesema kuwa Serikali inawajali na kuwathamini wananchi wake ndio maana inapambana kuzitatua changamoto za Maji.

Na Bernadetha Mwakilabi.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Kongwa Dkt. Omary Nkullo amesema kuwa ni muhimu kuboresha huduma za maji kwa kuwa maji ni uhai kwa binadamu.

Nkullo ameeleza hayo katika hafla fupi ya kushuhudia zoezi la makabidhiano ya miradi ya maji iliyopo katika kata tatu za Sejeli, Sagara na Ugogoni  iliyokuwa ikisimamiwa na wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini RUWASA kwenda kwa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Dodoma DUWASA lengo likiwa ni kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji wilayani humo.

Sauti ya Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Kongwa .

Akiongea mgeni rasmi katika hafla hiyo mkuu wa wilaya Kongwa Mheshimiwa Remidius Mwema Emmanuel amewaagiza viongozi wa Kata husika kuitisha mikutano ya wananchi na kuwapa taarifa sahihi juu ya mabadiliko hayo ya usimamizi wa miradi ya maji ili kuondoa sintofahamu kwa wananchi.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Kongwa.

Akisoma taarifa ya upatikanaji wa maji katika maeneo yanayokabidhiwa DUWASA kaimu meneja RUWASA wilaya Kongwa Mhandisi Mohamed Ally amesema wanakabidhi nyaraka za miradi ya maji za kata zote tatu ikiwemo miundombinu na akaunti za fedha za Maji.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Kongwa Dr Omary Nkullo akizungumza wakati wa hafla fupi ya kushuhudia zoezi la makabidhiano ya miradi ya maji kati ya RUWASA NA DUWASA mapema Leo. Picha na Bernadetha Mwakilabi.

Aidha Mhandisi Ally ameeleza changamoto katika miradi ya maji kuwa ni pamoja na kukosekana kwa miundombinu ya maji katika baadhi ya maeneo  Hali inayopelekea wananchi kutumia maji yasiyo safi na salama na kumia muda mwingi kutafuta maji na baadhi ya miradi kupitwa na kipindi cha usanifu ambapo changamoto hizo zimetatuliwa.

Sauti ya kaimu meneja RUWASA

Nae Meneja wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Dodoma DUWASA wilaya ya Kongwa Mhandisi Amrani Gamma ameeleza kuwa wataangalia namna ya kuhuisha miradi iliyoisha muda ili kumtua mama ndoo kichwani.

Sauti ya Meneja wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Dodoma DUWASA .