Dodoma FM

Viongozi wa vijiji kuhamasisha wananchi kutatua changamoto za elimu

21 September 2023, 4:08 pm

Picha ni wadau wa elimu , watendaji wa vijiji na waratibu wakiwa katika kikao cha upokeaji wa taarifa ya uchechemuzi na utetezi kwenye sekta ya elimu wilaya ya Chamwino. Picha na Seleman Kodima.

Mradi huo unatekelezwa wilaya ya chamwino katika Kata nne.

Na Seleman Kodima.

Viongozi wa Serikali za vijiji wametakiwa kutumia njia mbadala ya kuhamasisha wananchi ili waweze kutatua changamoto zilizopo katika sekta ya elimu ikiwemo miundombinu ya elimu.

Wito huo umetolewa na Afisa Utumishi wilaya ya Chamwino wakati akizungumza katika kikao cha upokeaji wa taarifa ya uchechemuzi na utetezi kwenye sekta ya Elimu wilaya ya Chamwino kilichofanyika ukumbi wa kilimanjaro Halmashauri ya Chamwino.

Aidha amewataka watendaji wa vijiji na madiwani kutumia mbinu ya kuwahamasisha wananchi kumalizia baadhi ya maboma ya shule ambayo yanasubiri nguvu ya serikali ili kutatua changamoto katika sekta ya elimu.

Sauti ya Afisa Utumishi wilaya ya Chamwino .

Awali akisoma taarifa Mjumbe wa kamati iliyoandaa taarifa hiyo, ameanisha baadhi ya Mambo waliyobaini kuwa ni pamoja na miundombinu ya elimu, vifaa vya kujifunzia pamoja na suala la chakula shuleni.

Sauti ya Mjumbe wa kamati.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati a Huduma za Jamii ambaye ni Diwani wa Kata ya Idifu, Simon Kawea amemuomba afisa elimu msingi wilaya ya chamwino kuandaa mpango wenye kuonesha maboma ya shule yaliyokaa muda mrefu ili taarifa zake zifikishwe kwa wabunge .

Sauti ya Simon Kawea .
Picha na Mkurugenzi wa Shirika la Afnet Bi. Joy Njelango akiongea katika kikao hicho. Picha na Seleman Kodima.

Nae Mkurugenzi wa Shirika la Afnet Bi. Joy Njelango amesema shirika hilo limekuwa likitoa Semina mbalimbali zenye lengo la kuzikumbusha Kamati za Shule, Viongozi na Wadau wa Elimu kuhakikisha wanashiriki katika utatuzi wa changamoto katika sekta ya elimu na kuhakikisha utoaji wa Elimu bora unazingatiwa.

Sauti ya Bi. Joy Njelango.

Shirika la Afnet kwa kushirikiana na shirika la Foundation for Civil Society (FCS) wanatekeleza mradi wa kuwajengea uwezo jamii ili kuongeza  kiwango cha ushiriki wa kusimamia serikali  kuwajibika katika utoaji wa Elimu bora kwa Shule za Umma.