Dodoma FM

Asasi za kiraia nchini zajadili mchango wake katika maendeleo ya nchi

25 October 2021, 12:46 pm

Na;Mindi Joseph.

Asasi za Kirai Nchini leo zimeketi pamoja katika mdahalo wa kujadili Mchango wake katika maendeleo ya Nchi na uchumi katika kuongeza pato la taifa na kupunguza umasikini kwa wananchi.

Akizungumza leo katika Mdahalo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society Bwana Francis Kiwanga amesema mchango unaotolewa na asasi za kirai katika kuongeza pato la taifa ni mkubwa hivyo AZAKI zinapaswa kubaki katika njia inayostahili.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Anna Henga amesema kuwa asasi za kiraia zimekuwa na mchango mkubwa katika utawala wa sheria ikiwa katika mabadailiko ya sheria mbalimbali nchini.

Aidha ameongeza kuwa endapo asasi za kiraia zitakuwa haziwajibiki vyema watakaoathirika ni wananchi ambapo itawapa wakati mgumu kupata uchambuzi wa kina kuhusu masuala mbalimbali.

Wiki ya Azaki 2021 bado inaendelea jijini Dodoma na leo Mdahalo wa kwanza umefanyika katika ukumbi wa royal village ambapo kesho pia unatarajiwa kuendelea.