Dodoma FM

Elimu ya TEHAMA yachochea idadi ya wasichana nyanja ya teknolojia

13 June 2023, 1:55 pm

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Mnadani wanasema elimu hiyo imekuwa chachu kwao kujifunza mambo mengi ya Teknolojia.Picha na Mindi Joseph.

Na Mindi Joseph.

Wanafunzi wa kike wamesema uwepo wa elimu ya TEHAMA inayotolewa na wadau imechochea kuongeza idadi ya wasichana kwenye nyanja ya teknolojia.

Taswira ya habari imezungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Mnadani sekondari wamesema elimu hiyo imekuwa chachu kwao katika kutimiza malengo yao.

Sauti za wanafunzi.
Elimu hii ya Tehama inawavuta wasichana wengi kujifunza elimu ya Teknolojia. Picha na Mindi Joseph.

Mwantumu Hussein Mmbaga ni mwalimu muwezashaji anasema kwa kawaida watoto wa kike wanaona masomo ya sanyansi ni Magumu.

Sauti ya Mwalimu.

Wanafunzi zaidi ya elfu 1830 nchini kupitia programu ya Code Like a Girl wamenufaika na elimu huyo kama anavyozungumza Mkuu kanda ya kati Vodacom Joseph Sayi.

Sauti ya Mkuu kanda ya kati Vodacom.