Dodoma FM

Dodoma wafurahishwa ongezeko la mtama sokoni

29 August 2023, 4:32 pm

Picha ni zao la mtama likiwa limevunwa tayari. Picha na Tadio.

Kutokana na Shirika la Afya , mtama umeweza kuwa chakula muhimu katika kupambana  na changamoto ya udumavu pamoja na  unyafunzi kwa watoto.

Na Astedi Bambora.

Upatikanaji wa zao la mtama kwa wingi katika soko kuu la majengo Jijini Dodoma kumewanufaisha wananchi  wengi .

Wakizungumza na Taswira ya Habari, baadhi ya wananchi wamesema kuwa kutokana na zao hilo kupatikana kwa wingi kumerahisisha hali ya upatikanaji wa chakula na hapa wanabainisha  matumizi mbalimbali ya zao hilo.

Sauti za wananchi.

Taswira ya Habari imezungumza na Bw. Fadhiri Saidi ambaye ni mfanyabiashara wa zao hilo Soko kuu la Majengo amethibisha kuwa Mtama umekuwa unapatikana kwa wingi hasa Dodoma vijijini hali ambayo imesababisha Mtama kusafirishwa hadi nje ya nchi.

Sauti ya Bw. Fadhiri Saidi .

Nao baadhi ya wananchi  wameshauri kuwa jamii ijitahidi kulima Mtama kwani unahimili ukamewa Mvua chache hata hivyo soko lake limekuwa linapanda zaidi.

Sauti za wananchi.