Dodoma FM

Watumishi wa Afya waaswa kuepuka uchepushaji wa dawa zenye asili ya kulevya

11 May 2023, 5:06 pm

Kaimu Mganga Mkuu Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma katika ufunguzi wa mafunzo ya wasimamizi wa dawa tiba zenye asili ya kulevya yaliofanyika Jijini Dodoma.Picha na Yussuph Hassan.

Mafunzo ya wasimamizi wa dawa tiba zenye asili ya kulevya yamehusisha wataalamu wa afya kutoka vituo mbalimbali Dodoma lengo ikiwa kuhakikisha dawa hizo zinaendelea kutumika katika lengo lako sahihi la kutibu.

Na Yussuph Hassan.

Wito umetolewa kwa watumishi wa afya kuepuka vishawishi  vitakavyosababisha uchepushwaji wa dawa zenye asili ya kulevya ili kuokoa nchi dhidi ya wimbi la kutibu waraibu wa dawa za hizo.

Wito huo umetolewa na Nelson Bukuru Kaimu Mganga Mkuu Hospitali ya rufaa ya Dodoma General katika ufunguzi wa mafunzo ya wasimamizi wa dawa tiba zenye asili ya kulevya yaliofanyika Jijini Dodoma.

Dkt Nelson amesema kuwa  dawa  zenye lengo la kutibu zinapotumika tofauti zina athari kubwa kwa jamii.

Sauti ya Dkt Nelson.
Benedict Brash Kaimu Meneja TMDA kanda ya kati . Picha na Yussuph Hassan.

Kwa upande wake Benedict Brash Kaimu Meneja TMDA kanda ya kati  amesema mafunzo hayo yataongeza ufanisi kwa wataalamu wa afya.

Sauti ya Kaimu Meneja TMDA.

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo walikuwa na haya ya kusema.

Sauti za washiriki.