Dodoma FM

Wananchi washiriki maendeleo ya kata Mparanga

7 December 2022, 11:29 am

Na ;Victor Chigwada.                                                                                      Kuongezeka kwa elimu  ya ushiriki wa maendeleo katika   jamii imesaidia kuongeza nguvu kwa Serikali juu ya utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazo wazunguka wananchi

Hayo yanajiri baada ya wananchi wa Kata ya Mpalanga kushiriki pamoja kukusanya fedha na kufanikiwa kujenga maabara katika shule ya sekondari kijijini hapo .

Wakizungumza na taswara ya habari baadhi ya wananchi hao wameiomba serikali kuunga mkono jitihada hizo ili waweze kukamilisha ujenzi huo

.

Mwenyekiti wa kijiji cha Mpalanga Bw.Mnyukwa Sakaila amekiri kuwepo kwa majengo kadhaa kwa upande wa shule ya sekondari pomoja na shule shikizi ambayo yanahitaji nguvu ya ukamilishwaji

.

Naye diwani wa Kata ya Mpalanga Bw.Baraka Ndahani ameeleza baadhi ya miradi ya ujenzi  iliyotekelezwa ikiwa ni pamoja na elimu ,ujenzi wa maabala,matundu ya vyoo pamoja na vyumba vya madarasa

.

Ndahani ameongeza kuwa tayari Serikali imesha anza kuunga mkono baadhi ya jitihada za wananchi ili ukamilishaji wa miradi ya shuleni ndani ya kata hiyo

.