Dodoma FM

Jamii imetakiwa kushiri kikamilifu katika kupiga vita ukatili wa kijinsia

27 May 2021, 2:32 pm

Na; Thadei Tesha.

Jamii imetakiwa kushirikiana kwa karibu na Serikali katika vita dhidi ya ukatili wa kijinsia zikiwemo mimba kwa wanafunzi.

Wakizungumza na taswira ya habari baadhi ya wanafunzi wa kike wa shule mbalimbali jijini hapa wamesema miongoni mwa sababu zinazochangia kuendeleza mimba kwa wanafunzi ni kukosekana kwa ushirikiano wa kutosha baina ya Serikali na jamii.

Naye afisa ustawi wa jamii wa jiji la Dodoma Bi.fauzia Mohamed amesema ili kupunguza vitendo vya ukatili kwa watoto pamoja na wanafunzi wazazi wanapaswa kuwasimamia kikamilifu ili kutokomeza vitendo hivyo.

Hatua hii inakuja siku moja baada ya jeshi la Polisi Mkoani Dodoma kuwakamata watu wawili kwa tuhuma za kuwapa mimba wanafunzi ambapo wanatarajiwa kufikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika.