Dodoma FM

Wananchi waomba kupatiwa elimu utunzaji wa macho

20 July 2023, 7:39 pm

Wananchi hao wanadai kuwa hawana elimu ya kutosha juu ya umuhimu wa kupima macho hivyo kusababisha watu wengi kupata changamoto ya macho. Picha na Aisha Shaban.

Kwa mujibu wa wataalam wa afya ya macho wanasema kuwa upo umuhimu mkubwa kwa watu kuwa na mazoea ya kupima afya ya macho mara kwa mara kutokana na macho kuwa moja ya kiungo muhimu katika utendaji wa kazi wa kiumbe hai.

Na Aisha Shaban

Baadhi ya wananchi jijini Dodoma wameomba taasisi zinazohusika na utoaji wa huduma za afya kuendelea kutoa elimu zaidi kwa jamii juu ya umuhimu wa watu kupima afya ya macho.

Wameyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati wakizungumza na kituo hiki na kukiri baadhi yao kuwa hawana elimu ya kutosha juu ya umuhimu wa kupima macho na kusababisha watu wengi kupata changamoto huku suala la gharama za matibabu likitajwa kuwa juu.

Sauti za wananchi.
Wataalam wanasema upo umuhimu mkubwa kwa watu kuwa na mazoea ya kupima afya ya macho mara kwa mara .Picha na Aisha Shaban.

Dodoma Tv imefanya mahojiano na daktari wa macho kutoka hapa jijini Dodoma Dk Salum salum ambapo kwanza nimeanza kwa kumuuliza je ni upi umuhimu wa kupima afya ya macho?

Sauti ya Daktari wa macho.