Dodoma FM

Wafahamu Maadui walio ibuka baada ya ujinga , maradhi na umaskini

24 April 2024, 6:48 pm

Mashindano hayo yalianza kwa Mara ya kwanza Mwaka 2022 chini ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma.Picha na Google.

Mashindano ya mdahalo kwa wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo Dodoma yanahusisha wanachama wa klabu za wapinga Rushwa kutoka shule za msingi, sekondari na vyuo.

Na Seleman Kodima.
Serikali imesema baada ya kufanikiwa kupambana na maadui watatu ambao ni Ujinga, Maradhi na Umasikini hali imebadilika na kuibuka kwa maadui wengi ikiwamo Rushwa, Madawa ya Kulevya, maadili na utawala Bora.
Hayo yamesemwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe George Simbachawene wakati akifungua mashindano ya mdahalo wa wanafunzi wa shule za Msingi, sekondari na Vyuo yaliyoandaliwa na ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Dodoma kwa ushirikiano na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Dodoma, Tume ya haki za Binadamu, Taasisi ya kuzuia na kudhibiti dawa za kule vya Dodoma.

Sauti ya Mhe George Simbachawene .

Aidha amewapongeza waandaji na waasisi wa mdahalo huo kwa kuanzisha jambo hilo lenye lengo la kutoa elimu ambayo itasaidia kuzuia vitendo vya rushwa, Matumizi ya Dawa za kulevya na kusisitiza utawala bora katika jamii.

Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amempongeza mkuu wa wilaya ya Dodoma kwa kutekeleza kwa vitendo dhamira ya kampeni ya kero yangu, Wajibu wangu kwa kuandaa mdahalo huo wenye kufikisha elimu ili kusaidia kuzuia vitendo vya Rushwa.
Video Rosemary &Takukuru