Dodoma FM

Wanawake Mnadani wazungumzia miaka mitatu ya Rais Samia

27 March 2024, 3:51 pm

Picha ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt Samia Suluhu Hassan. Picha na google.

Itakumbukwa kuwa Rais dkt Samia Suluhu Hassan ndie Rais wa kwanza mwanamke hapa nchini Tanzania na Afrika Mashariki ambapo aliapishwa rasmi march 19 mwaka 2021.

Na Mariam Matundu.
Ikiwa ni miaka mitatu tangu Rais Samia aingie madarakani maendeleo katika sekta mbalimbali yameonekana huku baadhi ya sekta zikipiga hatua zaidi katika kuboresha huduma kwa wananchi.

Taswira ya habari leo imefika mtaa wa Mnadani hapa Jijini Dodoma kuzungumza na wanawake ili kujua ni nini wanajivunia kutoka kwa Rais Dkt Samia kwa kipindi hiki cha miaka miatatu?

Sauti za Wanawake.

Hayo ni baadhi ya mambo yaliyofanywa na serikali chini ya uongozi wa Rais Samia ambayo wanawake wa mtaa huu wameyaona kama manufaa ,lakini bado wanatamani kuboresha zaidi katika mikopo ya kinamama,ajira pamoja na suala la uongozi .

Sauti za Wanawake.