Dodoma FM

Wananchi watakiwa kuwa makini na matumizi ya pilipili kupita kawaida

22 July 2026, 16:29

Je ni makundi gani yanapaswa kuwa makini na matumizi ya pilipili.Picha na Mtandao.

Hivyo, pamoja na kuleta ladha kwenye chakula, matumizi sahihi ya pilipili yanaweza kuwa na manufaa kiafya, huku ukizingatia kiasi kinachofaa kulingana na hali ya mwili.

Na Husna Munis.

Wananchi wametakiwa  kuwa makini na matumizi ya pilipili, hususan watu wenye matatizo mbalimbali ya kiafya, huku wataalam wa afya wakisisitiza ulaji wa pilipili kwa kiwango cha kawaida.

Kwa baadhi ya watu, chakula hakikamiliki bila pilipili kutokana na ukali wake unaoongeza ladha. Hata hivyo, licha ya kuwa pilipili ni kiungo kinachopendwa na wengi, lakini si salama kwa kila mtu kwa kiwango sawa, kwani kwa baadhi ya watu inaweza kusababisha madhara kiafya.

Lakini ni makundi gani yanapaswa kuwa makini na matumizi ya pilipili? Daktari Albert Martine kutoka mkoani Shinyanga anafafanua zaidi.

Sauti ya Daktari Albert Martine

Pamoja na ukali wake, pilipili pia ina faida mbalimbali mwilini inapoliwa kwa kiasi. Dkt. Albert Martine anaeleza namna kiungo hiki kinavyoweza kuwa na mchango chanya katika afya ya binadamu.

Sauti ya Daktari Albert Martine

Kiasili, pilipili ina kiambato kinachojulikana kama capsaicin, ambacho husaidia kuongeza joto la mwili, kuchochea uchomaji wa mafuta, kupambana na baadhi ya bakteria na kusaidia udhibiti wa kiwango cha sukari mwilini.