Dodoma FM

Walio kosa nafasi ya kusoma wahimizwa kurejea elimu ya watu wazima

24 August 2026, 16:54

Serikali imepokea na kuelekeza zaidi ya Sh22 bilioni mwaka 2026 katika kuimarisha miundombinu ya elimu. Picha na Anwary Shabani.

Serikali imewataka wananchi kutumia fursa hizo, kwa kuwa elimu haina umri wala mwisho na inaweza kuwa msingi wa kujenga maisha ya kujitegemea.

Na Anwary Shabani.

Wananchi waliokosa nafasi ya kusoma au waliokatisha masomo mkoani Dodoma wametakiwa kuendelea kupata fursa ya kurejea katika elimu na kujifunza ujuzi wa kujiajiri, kupitia programu za elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi.

Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma, Kiduma Mageni, amesema Serikali imepokea na kuelekeza zaidi ya Sh22 bilioni mwaka 2026 katika kuimarisha miundombinu ya elimu, ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha wananchi wanapata fursa ya elimu na ujuzi unaoweza kuwasaidia kukabiliana na changamoto za ajira na umaskini.

Nae Afisa Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi Mkoa wa Dodoma, Borase Chibula, amesema zaidi ya wananchi 2,000 wananufaika na programu hizo, zikiwemo MUKEJA na MEMKWA, huku wengine wakipata mafunzo ya uashi, umeme, uchoraji, upishi na kilimo.

Manufaa hayo yanaonekana kwa Bi. Magreth Boma, anayesema MUKEJA imemwezesha kujifunza kilimo cha uyoga, huku Ramadhani John, mwanafunzi wa MEMKWA, akisema programu hiyo imempa

Sauti na Anwary Shabani.