Dodoma FM

Madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani kuchukuliwa hatua

30 September 2026, 16:35

Picha ni mwananchi akizungumza na dodoma fm redio akitoa maoni yake kuhusu usalama wa barabarani na madereva kuchukuliwa hatua. Picha na Dodoma fm.

Wakati suala la mgomo wa madereva likiendelea kuibua mijadala kuhusu usafiri wa abiria, mjadala mwingine umeibuka kuhusu namna ya kukabiliana na madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani, huku wito ukitolewa kwa hatua za kinidhamu kwenda sambamba na elimu.

Na Daniel Njau.

Licha ya mjadala kuhusu mgomo wa madereva, suala la usalama barabarani limeibuka upya, huku wito ukitolewa na wananchi kuimba serikali kuhusika na madereva wanaokiuka sheria kuchukuliwa hatua za kinidhamu sambamba na kupewa elimu ya usalama barabarani.

Baadhi ya wananchi wameunga mkono hatua ya kupunguza alama kwa madereva wanaokiuka sheria, wakisema hatua hiyo inaweza kuwasaidia kutambua wajibu wao na kujifunza kutokana na makosa.

Hata hivyo, wengine wamependekeza kupunguzwa kwa ukali wa adhabu hizo ili kuepusha usumbufu kwa abiria wanaotegemea usafiri wa kwenda mikoa mbalimbali.

Akizungumza kuhusu changamoto hiyo, Bwana Adam Lameck, dereva wa magari yaendayo mikoani, amesema baadhi ya wamiliki wa magari pamoja na madereva hawazingatii ipasavyo sheria za barabarani. Amesema elimu kwa madereva na ukaguzi wa magari kabla ya kuanza safari ni muhimu katika kuimarisha usalama.

Amesema utekelezaji wa sheria unapaswa kwenda sambamba na elimu kwa madereva na wamiliki wa magari, hatua ambayo amesema inaweza kusaidia kupunguza ukiukwaji wa kanuni za barabarani na kuongeza usalama wa abiria.

Simulizi na Daniel Njau.