Dodoma FM

Ukosefu wa vitambulisho vya NIDA wa wanyima vijana fursa za mikopo

13 November 2026, 16:29

Picha nai mfano wa kitambulisho cha taifa kinachotolewa na NIDA. Picna na NIDA.

Hivi karibu Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Ayoub Mohammed Mahmoud akiji swali lililo ulizwa Bungeni na na Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kusini, Mhandisi Fadhili Chilombe alisema Serikali imetumia shilingi bilioni 1.06 katika awamu ya kwanza ya kusogeza huduma za usajili wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA) karibu na wananchi, ikiwemo katika maeneo ya vijijini.

Na Victory Chigwada.

Baadhi ya vijana katika Kata ya Mlowa barabarani wamelalamika kushindwa kufuatilia vitambulisho vya Taifa NIDA kutokana na ofisi za nida kuwa mbali hali inayo pelekea kukosa fursa mbalimbali .

Wakizungumzia changamoto hiyo vijana hao wamesema wanalazimika kusafiri kutoka eneo walipo hadi zilipo ofisi za Nida kufuata kimbulisho cha Taifa jambo linalo kwamisha vijana wengi kuwa na vitambulisho hivyo.

Aidha wamesema mzunguko uliopo wakati wa kufuatilia vitambulisho hivyo unapelekea kijana kukata tamaa na kuacha kufuatilia vitambulisho hivyo.

Mwenyekiti wa maendeleo Kata ya Mlowa barabarani Bw.Anjero Lukas amekiri uwepo wa changamoto ya vijana kukosa vitambulisho vya Taifa katika eneo hilp hivyo kupelekea kukosa mikopo ya Serikali inayotolewa na Halmashauri .

Lucas amesema kuwa hali hiyo imewawalazimu kuiomba mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA kupiga kambi katika Kata ya Mlowa barabarani ili wananchi waweze kupata vitambulisho hivyo kwa urahisi.

Alisema fedha hizo zimetumika katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027 na zimewezesha kuanza kwa huduma za usajili katika maeneo ya wananchi.

Simulizi na Victory Chigwada.