Wananchi wahimizwa kujenga utamaduni wa kupima afya
23 October 2026, 16:34

Jamii imetakiwa kujenga utaratibu wa kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara ili kubaini mapema viashiria vya magonjwa, kupata matibabu kwa wakati na kupunguza hatari ya kupata madhara makubwa yanayoweza kujitokeza kutokana na kuchelewa kugundua matatizo ya kiafya.
Na Daniel Njau.
Baadhi ya wananchi, wakiwemo vijana, wanasema kupima afya kunawasaidia kufahamu hali zao za kiafya na kuchukua hatua stahiki. Vijana hao wamewataka wananchi wengine kuzingatia uchunguzi wa afya hata wanapokuwa hawana dalili za ugonjwa.
Kwa upande wake, mmoja mwenye umri mkubwa anasema hana utaratibu wa kupima afya, isipokuwa anapohisi maumivu, ambapo hutumia dawa za kutuliza maumivu bila kufahamu chanzo cha tatizo.
Akizungumzia hali hiyo mtaalamu wa Afya, Daktari Milton Bernard anasema matumizi ya dawa bila ushauri wa wataalamu yanaweza kuchelewesha utambuzi wa magonjwa na kuongeza hatari ya kupata madhara makubwa.
Ameshauri jamii kupata ushauri wa kitaalamu kuhusu vipimo vinavyofaa na muda wa kuvifanya, badala ya kusubiri hadi dalili za ugonjwa zijitokeze.