Wananchi watakiwa kuunga mkono juhudi za usafi wa mazingira
19 October 2026, 16:54

Wananchi wamesema wako tayari kuendelea kushirikiana na serikali katika kuhakikisha usafi wa mazingira unakuwa wa kiwango cha juu.
Na Mariam Kasawa.
Wananchi wametakiwa kuendelea kushirikiana na serikali katika kudumisha usafi wa mazingira ili kuhakikisha Jiji la Dodoma linakuwa safi na salama .
Akizungumza wakati wa zoezi la usafi wa mazingira lililofanyika Jumamosi,Mwenyekiti wa Mtaa wa Mpamaa, Kata ya Miyuji bi, Hapines Joshua amesema kuwa ushirikiano kati ya wananchi na serikali ni muhimu katika kufanikisha juhudi za kuboresha usafi wa mazingira ambapo zoezi hilo litaendelea kufanyika kila siku katika maeneo mbalimbali, ikiwemo nyumba kwa nyumba.
Kwa upande wao wananchi wamesema wako tayari kuendelea kushirikiana na serikali katika kuhakikisha usafi wa mazingira unakuwa wa kiwango cha juu na kulifanya Jiji la Dodoma kuwa mfano wa usafi nchini.
Aidha, amewahimiza wananchi kuendeleza utamaduni wa kufanya usafi katika maeneo yao ya makazi na kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali zinazolenga kuboresha mazingira, akieleza kuwa jukumu la usafi linahitaji ushiriki wa kila mmoja.
Zoezi hilo la usafi wa mazingira ni sehemu ya juhudi za kuhamasisha wananchi kuimarisha usafi na kujiandaa na msimu wa mvua, kwa lengo la kupunguza hatari ya magonjwa yanayoweza kusababishwa na mazingira machafu na kuhakikisha Jiji la Dodoma linakuwa safi wakati wote.