Mwitikio wa vijana elimu ya uzazi wa mpango waongezeka Muungano
3 November 2026, 16:21

fursa ya elimu ya uzazi wapango inaongeza kuwa na utaalamu wa kupanga familia Kwa wenza na usalama Kwa Binti ambaye hajafikia maamuzi ya kubeba ujauzito .
Na Victor Chigwada.
Imeelezwa kuwa mwitikio wa vijana katika masuala ya elimu ya uzazi wa mpango umekuwa mkubwa tofauti na hapo awali .
Frolensia Msimbila mtaalamu wa afya katika zahanati ya Kijiji cha Muungano Wilayani Chamwino amekiri uwepo wa vijana wengi katika huduma ya uzazi wa mpango huku wakitumia fursa hiyo kuwashauri njia Bora za uzazi wa mpango pindi wafikapo katika eneo la huduma za afya
Bi.Msimbila ameendelea Kwa kuwapongeza vijana kutambua muhimu wa kupata elimu ya afya ya uzazi sambamba na kutumia njia za uzazi wa mpango kwani hali hiyo inatoa matumaini ya kuwa na familia Bora.
Nao baadhi ya vijana wamesema fursa ya elimu ya uzazi wapango inaongeza kuwa na utaalamu wa kupanga familia Kwa wenza na usalama Kwa Binti ambaye hajafikia maamuzi ya kubeba ujauzito .