Dodoma FM

Vijana balehe wapatiwe elimu ya afya ya uzazi

6 July 2026, 17:04

Ili kupunguza changamoto zinazotokea za afya ya uzazi kwa akina mama ni vema mabinti wakafundishwa mapema na kufahamu magonjwa yatokanayo na afya ya uzazi.Picha na Mtandao.

Pia amewataka wazazi hususani wa kike kukaa pamoja na mabinti zao kuwaeleza madhara ya mimba za mapema na namna ya kujilinda dhidi ya mimba hizo.

Na Jerome John.

Mabinti wenye umri wa balehe wameshauriwa kupata elimu ya afya ya uzazi ili ufahamu madhara na namna ya kujikinga na maradhi hayo.

Akizungmza na Taswira ya habari Daktari wa masuala ya uzazi Dkt. Suzan Babideli amesema kuwa ili kupunguza changamoto zinazotokea za afya ya uzazi kwa akina mama ni vema mabinti wakafundishwa mapema na kufahamu magonjwa pamoja na namna ya kujilinda dhidi ya magonjwa hayo.

Aidha amewashauri mabinti kuwa huru kuzungumza pindi wanapokutana na changamoto za afya ya uzazi na kuwaona madaktari ili kutatua changamoto hizo za kiafya.

Sauti ya Dkt. Suzan Babideli.

Vile vile Daktari Suzan amebainisha kuwa magonjwa ya afya ya uzazi kwa akina mama na mabinti ni pamoja na saratani ya mlango wa kizazi,ugonjwa wa uvimbe kwenye nyonga,saratani ya mfuko wa uzazi,kisonono,kaswende na mengineyo.