Wananchi iyoyo walia na umbali wa zahanati
14 August 2026, 16:25

Matonya Mtukamsihi mwenyekiti wa Kijiji Cha Muungano amekiri uwepo wa athari za kiafya Kwa wakazi wa kitongoji cha Iyoyo na vingine zaidi vitatu kutokana na umbali mrefu na ilipo zahanati. amesema Kwa kutumia nguvu za wananchi tayari wameanza ujenzi wa zahanati nyingine itakayo toa huduma Kwa vitongoji hivyo.
Na Victor Chigwada.
Wananchi wa Kitongoji Cha Iyoyo Kijiji Cha Muungano Wilaya ya Chamwino wamesema kukosekana Kwa zahanati ya karibu kitongoji hapo ni maumivu makubwa kwao pindi wanapohitaji kupata huduma za matibabu na uzazi Kwa akina mama.
Maumivu hayo yanatokana na kutembea kilomita kadha kufika zahanati ilipo Kijiji mama Cha Muungano, amesema kuwa changamoto hiyo inaathiri akina mama wajawazito, watoto na wananchi Kwa ujumla.
Huku msimu wa mvua ukiwa na mashaka Zaidi ya kushindwa kufika zahanati kutokana na ubovu wa barabara uliopo hivyo ni vyema Serikali kuongeza nguvu ya ujenzi wa zahanati ambayo wananchi wameanza nayo.