Dodoma FM

Uhifadhi sahihi wa mswaki watajwa kuwa muhimu kulinda afya ya kinywa

9 September 2026, 16:39

Ni muhimu wananchi kuzingatia usafi na uhifadhi sahihi wa mswaki baada ya matumizi. Picha na mtandao.

Wananchi wamehimizwa kuzingatia matumizi na uhifadhi sahihi wa mswaki kama sehemu ya utunzaji wa afya ya kinywa, pamoja na kuzingatia usafi wa meno kwa njia inayofaa ili kuepuka matatizo yanayoweza kujitokeza kutokana na matumizi yasiyo sahihi ya mswaki.

Na Elizabeth Mwinuka.

Uhifadhi na matumizi sahihi ya mswaki ni miongoni mwa hatua muhimu katika kulinda afya ya kinywa, huku matumizi yasiyo sahihi yakitajwa kuwa yanaweza kuathiri meno na fizi.

Baadhi ya wananchi wamesema wamekuwa wakitumia miswaki kila siku, lakini wakati mwingine hawazingatii namna sahihi ya kuitunza baada ya matumizi wala muda wa kuubadilisha.

Wamesema elimu zaidi inahitajika ili kufahamu namna bora ya kuhifadhi na kutumia mswaki.

Akizungumzia hali hiyo, Daktari wa Meno kutoka hospitali ya rufaa ya Temeke jijini Dar es salaam Dkt. Nestory Shirima amesema ni muhimu wananchi kuzingatia usafi na uhifadhi sahihi wa mswaki baada ya matumizi, ikiwemo kuuosha vizuri na kuuweka sehemu safi yenye hewa ili kupunguza uwezekano wa uchafu na vijidudu kujikusanya.

Aidha, Dr. Shirima ameeleza kuwa mswaki unatakiwa kutumika kwa kipindi kisichozidi miezi miwili kabla ya kubadilishwa, huku akiwashauri wananchi kuepuka kutumia nguvu kubwa wakati wa kusafisha meno kwa kuwa kufanya hivyo kunaweza kuharibu fizi.

Sauti na Elizabeth Mwinuka.